KWA UPANDE WA CAF CHAMPIONZ LIGI JUMAMOSI HII SAMATTA KUIONGOZA TP MAZEMBE UWANJA MWEUPE ALGERIA ##

TP Mazembe ya Congo DR Jumamosi Usiku itatinga Ugenini Stade du 8 Mai 1945 Mjini Algiers ukiwa mweupe bila Shabiki hata mmoja kuikabili Entente Sportive de Sétif – Algeria kwenye Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.

Hakuna Shabiki atakaeruhusiwa kuingia Uwanjani humo baada ya CAF kuifungia ES Setif kutokana na fujo za Mashabiki wake waliokuwa wakizifanya wakati wa Mechi za Makundi za Mashindano haya licha ya kuonywa na kupigwa Faini.

Hivi sasa TP Mazembe, wakiwa na Mastraika wawili wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, wamejichimbia huko Lizzy Sports Complex Mjini Accra, Nchini Ghana wakipiga Mazoezi makali yaliyoanza huko tangu Jumatatu.

Mapema Siku hiyo ya Jumamosi huko Kinshasa wenzao TP Mazembe, AS Vita Club, watakuwa Nyumbani kucheza Mechi nyingine ya kwanza ya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Club Sportif Sfaxien ya Tunisia.

Marudio ya Nusu Fainali hizi ni Septemba 27.

Jumamosi Septemba 20

17:30 AS Vita Club - Congo, DR v Club Sportif Sfaxien - Tunisia

22:00 Entente Sportive de Sétif - Algeria v TP Mazembe - Congo, DR

Marudiano

Jumamosi Septemba 27

16:00 TP Mazembe - Congo, DR v Entente Sportive de Sétif - Algeria

20:00 Club Sportif Sfaxien – Tunisia v AS Vita Club - Congo, DR
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment