MARIAM JUMA MKUU MPYA WA LUSHOTO AMELIPA KIPAUMBELE KWANZA SWALA LA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE KATIKA MWANZO WA MAJUKUMU YAKE ##

MKUU mpya wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, Mariam Juma amesema kipaumbele chake cha kwanza katika wilaya yake itakuwa katika masuala ya elimu hasa kwa watoto wa kike kutokana na kuwa ukimsomesha mtoto wa kike umeisaidia jamii nzima.
 

 Wito huo ulitolewa na Mkuu huyo wa wilaya mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula ambapo anachukua nafasi ya Alhaji Majid Mwanga aliyehamishiwa Bagamoyo mkoani Pwani.

Mhe Magalula Said Magalula akimwapisha Mhe. Mariam M. Juma kuwa  Mkuu wa Wilaya ya Lushoto katikati ya juma hili .

Amesema kuwa sababu kubwa ya kutoa kipaumbele hicho inatokana na ukweli kuwa ukimuwezesha mtoto wa kike kielimu itaweza kusambaa kwa haraka zaidi katika jamii inayomzunguka kutokana na wao kuwa karibu na familia zao.


Aidha amesema kuwa suala lengine ambalo atalipa kiupaumbele katika utendaji wake ni pamoja na masuala ya afya ya mama na mtoto kwa kujitahidi kutoa elimu kwao ili waweze kujifunguliwa hospitalini.



Hata hiyo amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na viongozi wengine  wa serikali kwenye wilaya hiyo ili kuweza kuchangia kasi ya maendeleo kwa wananchi kwenye maeneo mbalimbali wilayani humo.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment