TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 30
TAIFA STARS KUSHIRIKI COSAFA CUP.
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imethibitisha kushiriki michuano ya
kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Baraza la vyama
vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano
ya kombe la COSAFA inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi
Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya
makundi inatarajiwa kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa
za Afrika Mashariki moja kwa moja na kituo cha Luninga cha Supersport 4.
Taifa
Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi nane
zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia
hatua ya robo fainali, nchi nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni
Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles, Swaziland.
Katika
kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi
ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi
za Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo
zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa
viwango vya FIFA.
Kombe
la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka
Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi
wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.
Nchi
wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoros,
Lesotho, Madagascar, Malawi, Maurtius, Mayotte, Msumbuji,Namibia,
Reunion, Sychelles, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
SALAMU ZA RAMBIRAMBI.
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za
rambirambi kwa familia ya Bw. Nyama, kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu
Mohamed Nyama ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi ya
TFF kilichotokea jana kwao Nachingwea- Lindi.
Marehemu
Mohamed Nyama wakati wa uhai wake alikuwa mwamuzi wa daraja la kwanza
ambaye pia alitambuliwa na FIFA, Nyama anatarajiwa kuzikwa leo jioni
kwao Nachingwea mkoani Lindi na TFF itawakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji Bw. Athumani Kambi.
Katika
salam zake kwa familia ya Nyama, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa
miguu na watanzania Rais Malinzi amewapa pole wapenzi wa mpira wa miguu
nchini katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.
KILA LA KHERI AZAM, YANGA, KMKM NA POLISI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), limezitakia kila la kheri na
ushindi timu za Azam na Young Africans katika michezo yao ya marudiano
itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii .
Azam
FC itakuwa ugenini siku ya jumamosi mjini Khartoum, Sudan kucheza mchezo
wa marudiano na wenyeji timu ya El Merreikh ambapo katika mchezo wa
awali uliofanyika Chamazi jijini Dar es salaam Azam iliibuka na ushindi
wa mabao 2-0.
Jijini
Gaborone nchini Botswana katika kombe la Shirikisho, timu ya Young
Africans watacheza na wenyeji timu ya jeshi ya BDF XI siku ya ijumaa
katika mchezo wa marudiano pia, ambapo katika mechi ya awali Young
Africans iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mjini
Zanzibar KMKM wataikaribisha timu ya AL Hilal ya Sudan siku ya jumamosi
katika Uwanja wa Aman, huku kikosi hicho Maalum cha Kuzuia Magendo
kikihitaji ushindi wa kuanzia mabao 3-0 ili kuweza kusonga mbele,
kufuatia kupoteza mchezo wa kwanza Khartoum kwa mabao 2-0.
Timu
ya Polisi Zanzibar itakuwa mwenyeji wa timu ya FC Mounana kutoka nchini
Gabon siku ya jumapili katika mchezo wa kombe la shirikisho barani
Afrika,ikihitaji ushindi wa mabao 5-0 ili kufuzu hatua inayofuata baada
ya kupoteza mchezo wa awali kwa mabao 4-0.
Kwa
niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, famili ya mpira na
watanzania wote wanawatakia kila la kheri na ushindi katika michezo hiyo
ya marudiano ambapo timu hizo zitakua zikipeperusha bendera ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Home
MICHEZO
TAIFA STARS KUSHIRIKI COSAFA CUP # KILA LA KHERI AZAM, YANGA, KMKM NA POLISI # SALAMU ZA RAMBIRAMBI. ##
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment