TIMU YA AFRICAN SPORTS “WANAKIMANUMANU” KESHO INATARAJIA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA OLJORO JKT YA ARUSHA

TIMU ya African Sports “Wanakimanumanu” kesho  inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na Oljoro Jkt ya Arusha ikiwa ni kusaka makali ya kikosi chao kabla ya kuelekea Michuano ya Ligi daraja la kwanza itakayoanza Octba 12 mwaka huu hapa nchini.









Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mkoani hapa .

Ofisa Habari wa timu hiyo,Saidi Karsandas alisema kuwa maandalizi ya kuelekea michezo hiyo kwao yanaendelea vizuri na Oljoro watatua jijini Tanga (leo)jana kwa ajili ya mechi hiyo ambayo ni muhimu kwa timu zote kujiandaa na michuano hiyo.

Karsandas alisema kikosi cha timu hiyo kinaendelea na mazoezi yake kwenye uwanja wa shule ya sekondari Usagara wakiwinda na mashindano ya ligi daraja la kwanza lengo likiwa kushiriki kwa mafanikio ili waweze
kupata nafasi ya kucheza ligi kuu msimu ujao.

Alisema baada ya kumalizika mechi hiyo watacheza na Panoni FC ya Kilimanjaro kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kabla ya kuvaana na AfricanLyon ikiwa ni mechi ya ufunguzi wa michuano ya Ligi daraja la kwanza.




Akizungumzia hali ya kikosi hicho, Kocha Mkuu Ally Manyani alisema kuwa wachezaji wote wapo imara na hakuna majeruhi hata mmoja kitendo ambacho kinampa uhakika wa kuanza vema mashindano hayo.

Ofisa Habari hiyo alisema wanachama wa timu hiyo wanatarajia kuwa na kikao kitakachozungumzia masuala mbalimbali ya timu hiyo ikiwemo mkakati wao wa kuelekea michuano hayo
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment