Wakazi wawili wa kijiji cha Lomotio Wilayani hapa,wanashikiliwa na jeshi la polisi wakihusishwa na mauaji ya Kazenge Zakayo (20) aliyekufa kwa kuchomwa moto na kitu chenye ncha
kali.
kali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Frasser Kashai alisema jana kuwa mauaji hayo yalifanyika saa 1.00 jioni kijijini Lomotio kata ya Pagwi iliyopo tarafa ya Kwekivu.
Aliwataja wanaoshikiliwa na Polisi kuhusiana na tuhuma hizo kuwa ni Matatizo Mgongo (20) na Samwel Esay (22) ambaye ni mkulima kijijini hapo.
“Marehemu alikufa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni upande wa kushoto na watu wasiojulikana “alisema Kashai.
Alisema kufuatia mauaji hayo ,jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa hao ili waweze kusaidia uchunguzi na ili kuweza kuwanasa wengine zaidi.
0 comments:
Post a Comment