Mazoezi hayo yaliyoanza saa kumi jioni na kumalizika saa kumi na mbili jioni yakisimamiwa na Kocha Mkuu Yusuph Chippo akiwa na Msaidizi wake,Benard Mwalala sambamba na Mkurugenzi wa Ufundi Mohamed Kampira.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi hayo,Kocha Chippo amesema maandalizi ya kuelekea mechi hiyo yanaendelea vema na hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi.
Chippo amesema kutokana na juhudi zinazofanywa na wachezaji kwenye mazoezi hayo wanamatumaini makubwa ya kuchukua pointi tatu muhimu kwenye mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya kwanza kucheza nyumbani.
0 comments:
Post a Comment