Mkazi mmoja
wa kijiji cha Shume B kata ya DOCHI wilaya ya lushoto STEPHAN JOSEPH mwenye
umri wa miaka {38} ameuawa kikatili kwa kuchomwa kichwani na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana.
Akiongea na
waandishi wa habari kamanda
wa jeshi la polisi mkoani tanga FRAISER KASHAI amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mnamo
tarehe 5/10/2014 majira ya saa nne kamili usiku mwili wa mkulima huyo ulikutwa
kwenye shimo kandokando ya barabara ya mtae akiwa ameuawa.
| KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI TANGA FRAISER KASHAI |
Hata hivyo
kamanda kashai amesema kuwa mwili wa marehemu
umefanyiwa uchunguzi na madaktari na hatimaye kuukabidhiwa kwa ndugu wa
marehemu kwa ajili ya mazishi.
0 comments:
Post a Comment