STAIKA WA BASTIA HUKO FRANCE AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWEZI 1NA FAINI EURO 20,000 KWA KUMPIGA THIAGO MOTTA ##

Mwendesha Mashitaka huko France alitaka Straika huyo anaetoka Brazil mwenye Miaka 34 apewe Kifungo cha nje cha Miezi 8 lakini Mahakama ya Mjini Paris imeamua kumfunga Mwezi mmoja Jela.
Tukio hilo lilitokea mara baada ya Mechi ambayo PSG iliifunga Bastia 2-0 Uwanjani Parc des Princes na Brandao akamsubiri Thiago Motta akipita kwenye Ukumbi kuelekea Vyumba vya Kubadili Jezi ndipo alipomtwanga Kichwa.

Kipigo hicho kilimsababisha Thiago Motta avunjike Pua na Uongozi wa Soka Nchini France uliamua kumfungia Miezi 6.

Kwa mujibu wa Gazeti Le Parisien Mwanasheria wa Brandao hatakata Rufaa kupinga Kifungo cha Mwezi mmoja Jela kwa vile wanategemea Adhabu hiyo itageuzwa na kuwa ya kutumikia Jamii bure kwa kipindi maalum.

Mahakamani, Brandao alikiri Kosa lake lakini alikataa kwamba alikusudia kutenda kosa hilo.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment