NI DHAHIRI KUWA SHERMAN WA YANGA ANA NAFASI KUBWA YA KUKICHAPA JANGWANI BAADA YA KUFUZU VIPIMO VYA AFYA LEO ##

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Liberia, Kpah Sean Sherman amefuzu  vipimo vya afya na sasa yuko kwenye majadiliano ya kimkataba na  uongozi wa klabu ya Yanga SC.

Sherman akiwa na vifaa  maalumu  mwilini mwake  kwa ajili ya kucheki afya yake zoezi ambalo limefanyika leo
Sherman anatarajiwa kusaini Mkataba wa kujiunga na klabu ya Yanga  SC, baada ya awali kuwa amefikia makubaliano na uongozi wa klabu  hiyo akiwa Cyprus.

Kwa pamoja, Yanga SC na mchezaji huyo wana matumaini makubwa mambo  yatakwenda vizuri na watafunga ndoa ya mwaka mmoja.



Na iwapo zoezi la Mkataba litamalizika mapema, Sherman anaweza  kuingia kambini leo katika hoteli ya Landmark, Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Yanga SC kwa sasa ipo kambini katika hoteli ya Landmark, eneo la  Mbezi Beach, Dar es Salaam ikijiandaa na mechi ya Nani Mtani Jembe  2 Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Sherman anatarajiwa kucheza keshokutwa. 

Daktari wa Yanga SC, Sufiani Juma akiwa kazini .
Sherman mwenye umri wa miaka 22 ametua Yanga SC akitokea klabu ya  Cetinkaya ya Ligi Kuu ya Cyprus Kaskazini, ambako analazimika  kuvunja Mkataba wake uliobakiza miezi minne.

Alianza kuichezea Cetinkaya mwaka 2012, akitokea Duzkaya SK aliyoanza kuichezea mwaka 2010, akitokea Barrack YC ya nyumbani kwao, Liberia ambayo alianza kuichezea mwaka 2009.

Kpah Sean Sherman baada ya  zoezi hilo kukamilika
Sherman akifanikiwa kusaini Yanga SC, atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa dirisha la dogo baada ya kiungo mkabaji Mbrazil, Emerson de Oliviera Roque na mshambuliaji mzalendo, Danny Mrwanda aliyekuwa anacheza Vietnam.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Yanga SC kama  itamsajili Sherman mkali wa mabao katika Ligi ya Cyprus Kaskazini, italazimika kukata mchezaji mmoja wa kigeni ili ikidhi kanuni ya 

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotaka wageni watano tu.

Bila ya Sherman, tayari Yanga SC inao Wabrazil Emerson, Andrey Coutinho, Wanyarwanda Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite na Mganda  Hamisi Kiiza. 


Aidha, Sherman akisajiliwa Yanga SC atakuwa Mliberia wa pili  kucheza Tanzania, baada ya William Fahnbullar aliyewika Simba SC  kuanzia 1997 hadi 1999 alipohamia Kajumulo WS kabla ya kutimkia  Ulaya.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment