COASTAL UNION KUKIPIGA NA MOMBASA COMBAIN LEO ##


TIMU ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya”leo wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Mombasa Combain ikiwa ni kukipa makali kikosi hicho kabla ya kucheza mechi zake zinazofuata za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
 
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kuanzia saa kumi jioni ikiwemo wadau mbalimbali wa soka kutakiwa kujitokeza ili kuweza kushuhudia mchezo huo.
 
Ofisa Habari wa timu hiyo  amesema kuwa mechi hiyo ni sehemu ya kuhakikisha kikosi hicho kinajiimarisha zaidi kila idara kabla ya mchezo wake na Polisi Morogoro.
 
Hata hivyo aliwataka wapenzi wanachama na mashabiki wa soka kuhakikisha hawakosi fursa hii adimu kuja kuishuhudia timu yao ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani kabla ya kuanza mechi za Ligi kuu zinazofuata.
 
Wakati huo huo,Kikosi cha timu ya Coastal Union kinaendelea na mazoezi kila siku kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly na sasa kipo tayari kuweza kuikabili timu yoyote ile itakayokutana nayo na kuweza  kupata matokeo mazuri.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment