TANZANIA KUIVAA KENYA JUMAMOSI.
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) kesho
jumamosi itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, mchezo
utakaoanza majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Escape One Club Msasani
jijini Dar es salaam.
Wageni timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni kutoka nchini Kenya
wanatarajia kuwasili leo jioni jijini Dar es salaam, tayari kabisa kwa ajili ya
mchezo huo wa marudiano siku ya jumamosi na watafikia katika hoteli ya Saphire
iliyopo eneo la Gerezani – Kariakoo.
Katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini
Mombasa, timu ya Taifa ya Tanzania iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 3
dhidi ya wenyeji timu ya Taifa ya Kenya na kujitengenezea mazingira mazuri ya
kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Waamuzi wa mchezo huo watakua ni , Beye Mbokh kutoka Senegal,
mwamuzi wa pili ni Signate Youssouph (Senegal), mwamuzi wa tatu, Maolidy
Tsaralaza kutoka Madagascar, mtunza muda (time keeper) atakua Hachim Said
Nassur (Madagascar) na kamishina wa mchezo atakua Roch Henriette kutoka Visiwa
vya Shelisheli
Tayari waamuzi wa mchezo huo wameshawasili jijini Dar e salaam
tangu jana jioni tayari kwa mchezo huo, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania
itasonga mbele, itakutana na timu ya Taifa ya Misri kati ya Machi 7, 8 na
kurudiana kati ya Machi 13, 14, 2015.
Fainali za Soka la Ufukweni zinatarajiwa kufanayika mapema mwaka
huu katika Visiwa vya Shelisheli.
+++++++++++++++++++++++++++
TWIGA STARS KUINGIA KAMBINI JUMAPILI.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars),
Rogasian Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji thelathini (30) kitakachoingia
kambini siku ya jumapili kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya
Zambia mwezi Machi mwaka huu.
Twiga Stars ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume, imeingia moja kwa moja katika
hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo
wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Wachezaji walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma,
Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi,
Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu,
Fadhira Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia
Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai
Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa
Haji Vuai (JKU – Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment