Brazili jana aliikimbiza mchamchaka Ufaransa baada ya kuichabanga magoli matatu kwa moja.
Haikuwasaidia
Ufaransa kuanza kuona lango la Brazil katika dakika ya 21 kwa goli
lililofungwa na Raphael Varane kwani ni kama waliichokoza kundi la nyuki
kwani goli hilo lilirudishwa na Oscar dos Santos Emboaba Júnior katika
dakika ya 40, na hatimaye kushindiliwa magoli mengine mawili kupitia kwa
Neymar da Silva Santos, Júnior, na Luiz Gustavo na hivyo hadi mechi
hiyo inamalizika Brazil 3 Ufaransa 1.
Katika mechi nyingine za
kimataifa za kirafiki zilizochezwa hapo jana, Bahrain iligeuzuwa chapati
na Colombia pale waliposhindiliwa magoli 6 kwa mtungi huku Iran ikiwapa
darasa Chile kwa kuichabanga magoli mawili kwa nunge.
Leo kutakuwa na mechi nyingine za kimataifa za kirafiki ambapo moja kati ya hizo ni ile ya Canada kuwakaribisha Guatemala
MATOKEO YA MECHI ZA JANA:
MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI LEO:
MECHI NYINGINE ZA LEO RATIBA IPO HIVI:
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment