KUIONA STARS NA THE FLAMES YA MALAWI KIINGILIO CHA CHINI 5,000/ MALAWI TAYARI IMEWASILI MWANZA ##


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangza viingilio vya mchezo wa siku ya  jumapili kati ya Taifa Stars (Tanzania) dhidi ya The Flames (Malawi) utakaochezwa  kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuwa ni tsh. 5,000 mzunguko na tsh.  12,000 kwa jukwa kuu.

Kuelekea mchezo huo wa jumapili kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa CCM  Kirumba huku wachezaji wake wote wakiwa na ari na morali ya juu tayari kwa  kuwakabili the Flames.

Taifa Stars iliyo chini ya kocha mkuu Mart Nooij iliwasili jijini Mwanza siku ya  jumanne na kufikia katika hoteli ya La Kairo iliyopo eneo la Kirumba,ikiwa na kikosi  kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliopo  kwenye kalenda ya FIFA.

Maandalizi ya mchezo kwa upande wa Taifa Stars yamekamilika, timu imekua ikifanya  mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba ambao ndio uwanja utakaotumika kwa mchezo.

Wachezaji waliopo jijini Mwanza ni , Aishi Manula, Mwadini Ali, Shomari Kapombe,  Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Salim Mbonde, Haji Makame,  Hassan Isihaka na Abdi Banda.

Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Amri  Kiemba, Frank Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma Luizio, Thomas Ulimwengu na  Mbwana Samatta.

Kinara wa mabao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva hajachukuliwa kwenye  kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kitakachomenyana na Malawi Jumapili Uwanja wa  CCM Kirumba, Mwanza.

 Kocha Mholanzi, Mart Nooij amemuacha mchezaji huyo kwa sababu yupo kwenye kikosi cha pili cha Stars, maarufu kama Taifa Stars Maboresho ambacho kitakuwa na mechi mwezi ujao.

MALAWI YAWASILI MWANZA

Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) tayari imewasili leo jijini Mwanza majira ya  saa sita mchana, ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa  Stars siku ya jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Malawi imewasili ikiwa na kikosi chake kamili cha wachezaji 18 na kufikia katika  hotel ya JB Belimonte, wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka la kulipwa katika  nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.

Wachezaji wa kimataifa waliowasili ni nahodha Joseph Kamwendo (TP Mazembe -Congo  DR), Chimango Kayira (Costal de Soul - Msumbiji), Frank Banda (HBC Songo -  Msumbiji), Esau Kanyenda (Polokwane City - Afrika Kusini),  Harry Nyirenda (Black  Leopards - Afrika Kusini), Limbikani Mzava (Celtic - Afrika Kusini) Gerald Phiri  (Caps United - Zimbambwe

Wegine ni McDonald Harawa (Hoyale FC), Richard Chipuwa (Wanderers), Lucky Malata (Silver), John Lanjesi (Civo), Francis Mulimbika (Wanderers), John Banda (Blue  Eagle), Earnest Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti Chiriwa  (Red Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton).

Mkuu wa msafara ni Alexander Waya, Kocha mkuu Young Chimodzi, kocha msaidizi Jack  Chamangwana, kocha wa makipa Pillip Nyasulu, Daktari wa timu Levison Mwale, Meneja  wa timu Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinatarajiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni  katika uwanja wa CCM Kirumba, huku siku ya jumamosi wakipata nafasi ya kufanya  mazoezi tena kwenye uwanja huo wa mchezo.

Kesho jumamosi saa 5 kamili asubuhi kutafanyika mkutano na waandishi wa habari  katika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha wa Stars Mart Nooij  na kocha wa The Flames Young Chimodzi wataongelea maandilizi ya mchezo wao wa siku   ya jumapili.

 

Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment