MZEE YUSSUF NA ISHA MASHAUZI WATHIBITISHA RASMI MPAMBANO KATI JAHAZI NA MASHAUZI CLASSIC ##



 

Hatimaye wakurugenzi wa Mashauzi Classic na Jahazi Modern Taarab, wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kuthibitisha kuwepo kwa onyesho la pamoja la makundi hayo yenye nguvu katika muziki wa taarab.

Onyesho hilo litafanyika mwezi huu Jumapili tarehe 22 ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni.

Mkurugenzi wa Jahazi, Mzee Yussuf na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi, wamesema siku hiyo hatumwi mtoto dukani.

Wakiongea katika mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu jioni katika hotel ya Travertine Hotel, wakurugenzi hao ambao wote ni waimbaji nyota, wakasema onyesho hilo si mpambano lakini pia sio la masihara kwani kila bendi imejipanga kuhakikisha inaangusha burudani iliyokwenda shule.

Pichani juu kutoka kushoto ni: Meneja wa Mashauzi Classic Ismail Rashid, Isha Mashauzi, Mzee Yussuf na Seif Magwaru meneja wa Jahazi Modern Taarab.


Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment