STAND WAJIONGEZA SASA POINTI 21 BAADA YA GOLI MBILI MCHEZO UKIMALIZIWA LEO ##

Stand United imejiongeza kwakuibuka na  pointi tatu baada ya kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Mnigeria Chidiebere maarufu kama Chidi ndiye amefunga mabao yote mawili.
Chidi alifunga bao moja jana lakini mechi hiyo ikasimama katika dakika 80 kutokana na mvua kubwa.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ulianza jana na Stand United ikapata bao moja lililofungwa Chidiebele dakika ya 42. Chidiebele pia ndiye  aliyeifungia Stand bao pekee ikiilaza Simba 1-0 wiki iliyopita.

Kwa matokeo hayo, Stand inatimiza pointi 21 baada ya kucheza mechi 17 na kusogea nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiiteremsha Mtibwa Sugar nafasi ya nane.


 
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment