TANZANIA KUSHIRIKI MBIO ZA DUNIA ZA NYIKA MWEZI HUU TAREHE 28 ##


Wachezaji wa riadha wa Tanzania wameweka kambi ya mazoezi mkoani Arusha, wakifanya  mazoezi makali kwa ajili ya matayarisho ya kushiriki mbio za Nyika za dunia zitakazofanyika China Machi 28.

Chama cha riadha nchini Tanzania kimesema wanariadha wake wanaendelea vizuri na mazoezi chini ya kocha Francis John.

Kikosi cha wanariadha waliochaguliwa kinahusisha wale ambao walifanya vizuri dhidi ya Kenya katika mbio fupi (half marathon) za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi, Kilimanjaro.

Kenya ilitawala katika mbio ndefu (full Marathon) kwa kushinda kumi bora zote katika mbio hizo za Kilimanjaro Marathon.

Wakimbiaji wanaofanya mazoezi Arusha ni Fabian Nelson na Bazi John kutoka chuo cha Polisi cha Moshi.

Wengine ni Alphonce Erick wa Arusha, Emmanuel Giniki na Joseph Theophil.

Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment