
Kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Yanga walitangulia kupata Bao la Kwanza kwa Penati iliyotolewa baada ya Amos Makwaya wa Ruvu JKT kulinawa shuti la Simon Msuva na Msuva mwenyewe kufunga Penati hiyo katika Dakika ya 35.
Bao la Pili la Yanga lilifungwa Dakika ya 42 na Danny Mrwanda baada ya kazi njema ya Mrisho Ngassa na Msuva.
Kwenye Dakika ya 44 Ruvu JKT walipata Bao lao moja Mfungaji akiwa Samuel Kamuntu mpaka timu zinakwenda Mapumziko Yanga 2 Ruvu JKT 1.
Kipindi cha pili, Yanga SC walirejea na moto wao na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na Msuva, tena akimalizia pasi ya Ngassa. Msuva sasa ndiye anaongoza kwa mabao Ligi Kuu, 11 dhidi ya 10 ya Kavumbangu.
Yanga SC waliendelea kutawala mchezo na kupeleka mashambulizi zaidi langoni mwa JKT, lakini hawakuwa na bahati ya mabao zaidi.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 19, moja zaidi ya mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 36.
Kikosi cha JKT Ruvu; Benjamin Haule, Damas Makwaya, Ramadhani Shamte, Renatus Morris, Mohammed Fakhi, Nashon Naftali, Amos Mgisa/Ally Bilal dk58, Jabir Aziz, Samuel Kamuntu, Iddi Mbaga/Emmanuel Pius dk41 na Alex
Abel.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Juma ‘Makapu’, Salume Telela, Haruna Niyonzima/Nizar Khalfan dk 87, Danny Mrwanda/Hussein Javu dk72, Mrisho Ngassa na Simon Msuva.
LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Aprili 4
Mtibw Sugar v Stand United
Coastal Union v Tanzania Prisons
Ruvu Shooting v Ruvu JKT
Ndanda FC v Mbeya City
Kagera Sugar v Simba (Mechi kuchezwa Kambarage, Shinyanga)
0 comments:
Post a Comment