
Nitaanza
na mifano michache kunasheria mitandao zilizopendekeza kifungo cha maisha kwa
wahalifu mtandao nchini Uingereza. Na katika Kikao cha usalama mitandao
kilichopita mshiriki aliyekua nami meza kuu katika kuongoza moja ya kikao
aliyetokea “US Secret service” alipata kuainisha adhabu ya miaka kumi na sita
bado imeonekana ni ndogo na inashauriwa kuongezwa makali.
Aidha,
Nieleze ushauri wa kuhakiki sheria mitandao zinaboreshwa na kuwa kali zaidi ni
kutokana na athari ya uhalifu mtandao kua kubwa sana na imekua ikimgusa kila
mmoja wetu – Kwan nje ya nchi kila siku tumekua tukipata habari mpya ya matukio
ya kiuhalifu mtandao ambapo maelfu wamekua wakipoteza maisha, fedha na pia
ufaragha wao umekua ukitumiwa vibaya na wahalifu mtandao.
Tanzania
pia hatuko salama – Nimekua nikipata malalamiko mengi ya watu kudukuliwa
faragha zao, kuibiwa fedha nyingi sana na wengine kufikia hata kujitoa maisha
kwa kudalilisha mitandaoni.
Hayo
yote yamekua yakisukuma wataalam usalama mitandao kuumiza vichwa kuhakiki
wanakuja na mwarubaini wa uhalifu huu mtandao unaozidi kuota mbawa kila
kukicha. Hapo ndipo mengi yakawekwa sawa katika kukabiliana na hali hii ikiwa
ni pamoja na kukuza uelewa kwa watumiaji mtandao (Matumizi salama ya mitandao),
Kuzalisha na kuongezea uwezo kwa wataalam wa usalama mitandao, kuwa na sharia stahiki
za uhalifu mitandao, kukuza ushirikiano kutokana na uhalifu huu kutokua na
mipaka, kuhimiza kupatikana kwa takwimu sahihi za uhalifu mitandao ili kuweza
kutambua maeneo athirika zaidi.
Kwenye
hili la Sheria ni hatua nzuri sana ambapo Tanzania imefikia ili kuweza kurahisisha
mapambano dhidi ya uhalifu mtandao nchini na kuhakiki taifa linabaki salama
kimtandao. Naimani Kila mmoja wetu ukizingatia wote ni wahanga kwa namna moja
au nyingine ya uhalifu mtandao lazima tufurahie na kulipokea hili kwa mikono
miwili. Wataalam wa usalama mitandao wamefurahishwa sana na hatua hii yetu na
pongezi ni nyingi sana hadi sasa.
Kuondoa
hofu Watanzania naomba nieleze kwamba katika kuandaa muswada huu wataalam na
wadau mbali mbali walishirikishwa na badae kuvuka mipaka kwa wataalam kutoka
mataifa mbali mbali katika maswala haya ya usalama mitandao kutoa maoni yao na
kuboresha – Haikukomea hapo imepitia hatua kadhaa na hata kupelekea kauli yangu
niliyo itoa katika moja ya vikao vya wataalam wa usalama mitandao kueleza kuwa “
Hatua za kitaalam zimekwisha sasa ipo kwenye hatua za kisiasa kuweza kupatiwa Baraka
kabla ya kuwasilishwa bungeni” – Kauli ambayo wataalam
Nimepata
kufatilia kwa karibu kinachozungumzwa na wengi, Hofu kubwa nilizo ziona ambazo
nimeona nizitole ufafanuzi ni kama ifuatavyo: -
MOJA,
hofu kuwa uchunguzi wa makosa haya inaweza ikawa inakiuka faragha. Naomba nieleze
kuna anaefahamu faragha yake iko dhaifu kiasi gani mara tu anavyo kua
mtandaoni? Ni wazi kabisa unapaswa kujua faragha haiingi matatani tu kwa sababu
ya sharia hizi mtandao.
Uchunguzi
wowote wa uhalifu mitandao duniani kote unahusisha uangalizi wa kina hatua kwa
hatua kwa kila ushaidi wa kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupitia kwa karibu
kila chembe ya shaka ya kile kinachoweza kuonekana kinaweza kuwa na chembe ya
sababu ya uhalifu mtandao.
Uchunguzi
wa makosa ya digitali ni fani na ina maadili yake – Maadili ambayo yanasomewa
darasani. Maadili hayo yana hakiki mchunguzi anafata masharti na vigezo stahiki
vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kutotoa siri zisizoendana na uhalifu mtandao
unaochunguzwa pamoja na kuwasilisha ushahidi kwa mhusika pekee bila
kushirikisha kila mtu. Zaidi inawatu maalum si kila mtu anatakiwa kushiriki
katika uchunguzi wa uhalifu mtandao. Na hili kuna moja ya masharti yana sisitiza
kushirikisha idadi ndogo sana ya wachunguzi ni vyema zaidi.
MBILI,
kuna hofu kwanini makosa mtandao yanapatiwa ruhusa ya kuchunguzwa bila hata
kusubiri ruhusa ya mahakama? Ikumbukwe kuwa kwanza uhalifu mtandao unafanyika
kwa haraka sana na hauna mipaka. Ndio maana hili limeangaliwa sana na kuamua
kutoa ruhusa kwa wapelelezi teule wa makosa ya uhalifu mtandao kupewa fursa ya
kuazisha uchunguzi mara moja bila ya kungoja mahakama, Ikumbukwe kuna
kinachoitwa “search warrant” ambacho mchunguzi wa makosa mtandao anakua nacho nahii
inatolewa na kiongozi katika kitengo kinacho jihusisha na usalama mitandao
katika taifa husika. Kusisitiza hili kama pangetolewa ruhusa kusubiri protokali
za mahakama kufatwa kumbuka uhalifu mtandao unauwezekano mkubwa sana wa
kupotezwa ushaidi wake na kusababisha ugumu kwenye kufikia malengo.
TATU,
Hofu ya faragha ya kupekuliwa mawasiliano – Niulize kama unatumia mtandao
kuwasiliana vizuri hofu inatoka wapi kwenye hili. Kama unajua hunachembe ya
uhalifu mtandao katika mawasiliano yako sidahani kuna haja ya kua na hofu
kuchunguzwa. Na ikumbukwe yule aliyetiliwa mashaka pekee ndie anaye pekuliwa si
kila mmoja atapekuliwa mawasiliano yake. Hii iko kila mahali duniani sisi sio
wa kwanza.
Mimi
nadhani hofu kubwa tulitakiwa kuwa nayo ni kuhusu mamilioni ya pesa yanayo
potea katika mabenki yetu, athari za lugha za uchochezi kwenye mitandao, athari
za kuporomoka kwa maadili yetu, athari za mama na dada zetu kusambazwa picha
zao za uchi mitandaoni, athari za wasanii wetu kutopata mapato kutokana na watu
kuiba kazi zao mitandaoni, athari za kudukuliwa na wahalifu mitandao na taarifa
zetu kutumiwa vibaya, athari za kuogopa kufanya miamala ya kifedha kupitia simu
zetu, athari za kuogopa kuweka pesa benki inayo pelekea uchumi wa taifa
kuyumba, athari zilizombele yetu zinazoweza kupelekea kuhatarisha maisha (
Kufa) kupitia uhalifu mtandao na athari nyingine nyingi.
Ikumbukwe
athari ni kubwa sana za uhalifu mtandao na hofu kubwa tulipaswa tuwe nayo na
kwapamoja tuungane kuhakikisha sharia mtandao zinazidishwa makali na uchunguzi
wake unafanywa kwa kina na utaalam wa hali ya juu. Hili ndilo linapelekea
wataalam tunakutana mara kwa mara kuongezeana uwezo wa kuhakiki tuna tambua
mbinu mpya za uhali mtandao na kujinoa kujua namna ya kuchunguza na kuweza
kufikia malengo ya kudhibiti.
Wabunge
walionyesha hisia zao kutaka kupata ufumbuzi wa mabilioni ya pesa yanayopotea katika
mabenki na makampuni ya simu kupitia uhalifu mtandao – Wanapaswa kukumbuka
udhibiti unapaswa kwenda sambamba na kua na sheria madhubuti zinazoweza
kuhimili hali mbaya ya uhalifu mtandao nchini.
Naomba tu kusisitiza watanznaia kusoma na kuelewa na sio tu kufata mikumbo kwenye hili. Aidha, Hofu kubwa lazima iondoshe hofu ndogo. Nikiimanisha Uhalifu mtandao nitishio kubwa kuliko ugaidi na sheria zetu zanafanana kabisa na sheria nyingine za mataifa mbali mbali huku baadhi zikiwa kali zaidi kuliko tulizo nazo. Nimalizie kwa kutoa wito wa matumizi salama ya mitandao ili kujiepusha na kuingia matatani bila sababu za msingi. Huku nikiwatoa watanznaia hofu juu ya uchunguzi wa dhati wa makosa haya uanafanywa na hakuana atakae ingia matatani kama si muhusika.
CREDIT @ykileo.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment