DAIMOND PLATNUMZ NA RAIS KIKWETE WAMESHINDA TUZO ZA AFRICAN ACHIEVERS AWARDS ##


Diamond ameshinda tuzo nyingine kwenye tuzo za AFRICAN ACHIEVERS AWARDS 2015 zilizotolewa Afrika Kusini ambako pia Diamond alihudhuria.

Rais Jakaya Kikwete alishinda tuzo ya Uongozi bora na ikapokelewa na Dr. Asharose Migiro huku Diamond akichukua ya Artist of the Year kwa mujibu wa Salam.
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Tuzo hizi zimekua zikitolewa kwenye mataifa mbalimbali, mwaka huu 2015 zimetolewa Johannesburg South Africa huku za mwaka 2013 zikitolewa Nairobi Kenya, za mwaka 2014 zilitolewa Accra Ghana.
Ni tuzo ambazo zimekua zikitambua michango mbalimbali ya watu mbalimbali waliofanya bidii au kuleta mabadiliko kwenye jamii yao na zimekua zikitolewa kwenye vipengele mbalimbali kama kwa kampuni za simu, Mwanamichezo wa mwaka, Mwandishi wa habari wa mwaka, Kiongozi bora wa mwaka na nyingine.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment