Na Masanja Mabula –Pemba
……………………………………
Zaidi
ya mikarafuu 151 umeungua katika tukio la moto lililotokea janauri 22
mwaka huu katika bonde la Mkanyageni Shehia ya Mzambarauni Wilaya ya
Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba .
Jumla
ya eka tisa (9) za mashamba ya mikarafuu yameathiriwa zimehujumiwa
kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana na kusababisha hasara kuwa kwa
wamiliki ya mashamba hayo .

Amesema
kuwa kitendo cha kuchoma moto mashamba hayo ni kuhujumu uchumi wa nchi
pamoja na wananchi wake na kwamba serikali itahakikisha wanahusika
wanakamatwa na kufikishwa mahakamani .
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho ambacho
kinarudisha nyuma juhudi za serikali za kuliimarisha zao la karafuu
ambalo ndio uti wa mgogo wa uchumi wa Nchi.
“Serikali
haiwezi kuvifumbia macho vitendo vya kuhujumu uchumi wake , hivyo
naviomba vyombo vya sheria kufanya uchunguzi wa kina ili wahusika waweze
kupatikana na kufikishwa mahakamani ”alisisitiza.
Aidha
amefahamisha kwamba kuchomwa moto mashamba hayo ni hujuma za makusudi
zilizofanyika , kwani moto huo umetokea katika maeneo na mashamba
tofauti .
“Ukiangalia
jinsi moto ulivyotokea utabaini kwamba kuna hujuma za makusudi , moto
umetokea katika sehemu na maeneo tofauti , kitend hichi ni kudhoofisha
maendeleo ya nchi na wananchi wake ”alifahamisha.
Mmoja
wa wananchi wakaazi wa shehia hiyo Hamad Bakari Makame akizungumza na
mwandishi wa habari hizi amesema kwamba kitendo hicho kimesababisha
athari kubwa ya kiuchumi na kimazingira .
Alifahamisha
kwamba kutokana na bei za sasa ya zao la karafuu mkarafuu mmoja
unauwezo wa kuzalisha zaidi ya pishi ishirini sawa na zaidi ya shilingi
laki nne , na kuna zaidi ya mikarafuu 151 iliyoungua moto .
“Ni
hasara kubwa za kiuchumi na kimazingira , kwa kweli hali ya umaskini
kwa waliokuwa wakimiliki mikarafuu hii wimbi la umaskini linawanyemelea ,
tunataka uchunguzi ufanyike ”aliomba .
Aidha
amefahamisha kwamba katika Shamba la Mohammed Abdalla Chande mikaraafu
hamsini na nane (58) imeungua wakati katika shamba la Mani Abdalla
Chande (70) imeungua na mikaraafu 23 imeungua katika shamba la Serikali .
0 comments:
Post a Comment