Uchunguzi unaendelea baada ya picha ya ngono kuonyeshwa katika televisheni wakati wa maombolezi ya baba na mwanawe.
Ibada
ya Simon Lewis mwenye umri wa miaka 33 na mwanawe ilifanyika katika
eneo la kuchoma maiti la Cardiff Thornhill siku ya Jumatano.
Kiongozi
wa ibada hiyo Lionel Fanthorpe alisema kwamba kisa hicho kiliwaacha
waombolezaji wakiwa wamekasirika na mamlaka ya Cardif ikaomba msamaha
kwa familia kwa kisa hicho kisicho cha heshima.
Bwana Lewis na mwanawe walifariki kufuatia ajali mjini Cardif katika siku ya mkesha wa mwaka mpya.
Chombo
cha habari cha Media Wale kiliripoti madai kutoka kwa muombolezaji
ambaye hakutaka jina lake lijulikane kwamba picha za ngono zilionekana
katika runinga hiyo.
Runinga nne zilitumika kuonyesha risala za
rambi rambi na baraza hili lilisema kuwa televisheni ilioonyesha picha
hizo chafu ilikuwa imewekwa hivi majuzi.
''Tunajaribu kubaini
iwapo runinga hiyo mpya ambayo ni aina ya smart tv huenda ilinasa picha
hizo kwa bahati mbaya kupitia bluetooth ama kupitia wavu wa
Wi-fi,''alisema msemaji.
0 comments:
Post a Comment