OBAMA AONGEZEA KOREA KASKAZINI VIKWAZO

KoreaImage copyrightGetty
Image caption
Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia majaribio silaha za nyuklia na makombora hivi majuzi.
Msemaji wa ikulu ya White House amesema Marekani na jamii ya kimataifa hawatavumilia “shughuli haramu za nyuklia” zinazotekelezwa na Korea Kaskazini.
Awali, ikulu ya White House iliishutumu Korea Kaskazini ikisema inawatumia raia wa Marekani kama rahani katika juhudi za kuendeleza ajenda yake ya kisiasa.
Hii ni baada ya Korea Kaskazini kumhukumu mwanafunzi Mmarekani kifungo cha miaka 15 na kazi ngumu jela kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola.
WarmbierImage copyright
Image captionWarmbier alikiri kuiba bango hilo Februari
Bw Otto Warmbier, mwenye umri wa miaka 21, alikiri kuiba bango la kisiasa katika hoteli alimokuwa akikaa pamoja na kundi jingine la watalii mjini Pyongyang.
Marekani imeitaka Korea Kaskazini kumwachilia huru mwanafunzi huyo mara moja.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment