RAIS MAGUFULI AMEFANYA UTEUZI WA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI TATU ZA SERIKALI KWA MUJIBU WA MAMLAKA ALIYONAYO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anazidi kuendelea kuisuka Serikali yake ili iwe yenye ufanisi zaidi. Leo March 19 amefanya uteuzi ambao umeziba baadhi ya nafasi zilizokuwa wazi. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo. 

Rais Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Aidha Rais Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.

Rais Magufuli amemteua pia Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO). Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment