Moja kati ya wasanii wakike wanaouwakilisha mkoa wa Tanga kiburudani akiwa ni mmiliki halali wa wimbo wa mama aliomshirikisha _Kizzy Kiddy__Producer akiwa ni issam touch _@AIS music amepata fulsa ya kuzungumzia NA BONGOBAB KUBWA kwa siku ya leo akikumbushia swala zima la amani kama ambavyo linavyoendelea kuchukua sura mpya katika juma hili katika vyombo mbalimbali kwa kulitilia mkazo swala hili kupitia siku ya amani dunia .Ikikumbukwa kwamba WAKATI Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon anahimiza serikali duniani kutafuta chanzo cha kukosekana kwa amani na kuongezeka kwa watu wenye misimamo mikali, wasemaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa amani Duniani wameitaka serikali ya Tanzania kutupia macho makali mauaji ya albino nchini .
Huku wa upande wa msanii bivo roza akielezea kuwa "amani ni kitu muhimu sana hivyo kukidumisha ni muhimu sana kwasababu bila amani nadhani hata hivi tunavyoishi hivi sidhani kama tungeishi hivi kama tungekuwa hatuna amani japo kuwa tunaona kabisa kwamba kuna migogoro inaweza kutokea mbele ya safari ila inabidi tumuombe mungu ili amani yetu iendelee kudumu ameeleza bivo "
kama hujapata fulsa ya kuusikiliza wimbo wake aliomsifia mama na kumshukuru kama ambavyo wengi wana appreciate kuwa "hakuna kama mama "unaweza kuusikiliza hapo chini .
0 comments:
Post a Comment