COASTAL WAWASILI TANGA SALAMA WAAHIDI USHINDI KATIKA MECHI IJAYO DHIDI YA NDANDA ##

TIMU ya Coastal Union ya Tanga imerejea jijini Tanga jana usiku ikitokea Mkoani Mbeya ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mechi yao na Ndanda FC kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni muendelezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Jumamosi ijayo kwenye uwanja huo ambapo Coastal Unon wataingia uwanjani hapo mithili ya mbogo aliyejeruhiwa lengo kuweza kuhakikisha wanapata ushindi.

Kocha Mkuu wa Coastal Union,Yusuph Chippo amesema  kuwa wanamshukuru mungu kurejea salama jijini Tanga na hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi hivyo wapo tayari kuwakabili wapinzania wao hao.

Chippo alisema kuwa timu hiyo inatarajiwa kuanza mazoezi kesho ambapo asubuhi watafanya kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani na jioni kwenye viwanja wa shule ya sekondari Popatlaly wakiwa na wachezaji wao wote.

Alisema kuwa kubwa zaidi analilifanya hivi sasa ni kufanyia kazi mapungufu madogo madogo yaliyojitokeza kwenye mechi yao iliyopita dhidi ya Mbeya City iliyomaliza kwa wenyeji hao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine.

Akizungumzia hali ya wachezaji,Chippo alisema wachezaji wote wapo imara kuweza kuikabili Ndanda FC kwenye mechi yao ya Tatu kwenye michuano ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara itakayoendelea Jumamosi wiki hii.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment