WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI MKOANI TANGA ##

WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Tanga ambapo tukio la kwanza lilitokea kijiji cha Katurupesa kata ya Kwemkwazu wilayani Lushoto mkoani hapa kwa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 ambaye hakufahamika jina wala mahala anapoishi amegundulika amefariki dunia na mwili wake ukiwa umesogezwa kwenye kalvati la Daraja ikiwa baadhi ya viungo vyake sehemu ya kichwani sehemu za siri vikiwa vimeondolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai alithibitisha kutokea tukio hilo ambapo alisema limetokea Septemba 26 mwaka huu saa nane mchana eneo ha Katurupesa Kwemkwazu wilayani Lushoto mkoani Tanga ambapo mwili huo uligunduliwa na baadhi wa wasamaria wema.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA, FRESSER KASHAI


Alisema baada ya polisi kupata taarifa hizo walifanikiwa kufika eneo
la tukio ambapo waliuchukua mwili na kwenda kuuzikwa na wananchi baada
ya uchunguzi wa daktari kufanyika.

Kamanda Kashai alisema kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana
na watuhumiwa kuhusiana na tukio hilo bado hawajakamatwa wakati juhudi
za upelelezi ukiwa unaendelea ili kuweza kuwabaini wahusika.

Tukio la pili lilitokea Kijiji cha Kwangahu Kata ya Mkata Tarafa ya Mazingira wilayani Handeni lilihusisha mwendesha pikipiki Kiduo Rajabu (35) Mzigua akiwa anaendesha pikipiki yenye namba T.813 CAM aina ya Fekon akiwa amempakia Amiri Bakari (65) Mzigua mkulima wote wakiwa ni wakazi wa Mkonga wakielekea porini kuwinda wanyama na kila mmoja akiwa amebeba silaha yake aina ya Gobole.

Alisema kuwa walipofika kilima cha Lugala pikipiki ilishindwa kupanda mlima huo na kuanza kurudi nyuma na kuanguka chini ambapo katika tukio hilo silaha aliyokuwa ameibeba dereva alifyatua na kwa kuwa ilikuwa na baruti gololi na ilimjeruhi abiria Amiri Bakari ubavu wake wa kushoto na kusababisha kifo chake.

Kamanda Kashai alisema kuwa mtuhumiwa katika tukio hilo amekamatwa na upelelezi wa kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment