KIUNGO
Frank Domayo wa azam fc ataanza mazoezi mepesi Oktoba 1, mwaka huu baada ya
kumaliza muda wa mapumziko kufuatia kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja.
Domayo
aligundulika kuchanika vibaya nyama za paja, baada tu ya kusajiliwa na
Azam FC Juni mwaka huu, kufuatia kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili
Yanga SC.
Kufuatia
hali hiyo, alipelekwa Afrika Kusini alikofanyiwa opersheni na kutakiwa
kupumzika kwa miezi mitatu- na sasa yuko tayari kuanza jaribio la
kurejea uwanjani.
Aidha,
winga Joseph Kimwaga akiyekwenda kufanyiwa upasuaji pamoja na Domayo,
naye ameanza mazoezi mepesi tangu mwishoni mwa wiki.
Kimwaga
aliumia goti mwaka jana katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya
kuibuka vizuri kikosi cha kwanza cha Azam kufuatia kupandishwa kutoka
akademi.
Amekuwa
nje kwa muda wote akijaribu kutibiwa hapa nyumbani bila mafanikio kabla
ya kupelekwa Afrika Kusini, naye sasa anajaribu kurudi tena uwanjani.
Umaarufu
wa Kimwaga ulikuja baada ya kuifungia Azam FC bao la tatu katika
ushindi wa 3-2 dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita.
Kwa
upande mwingine, mshambuliaji John Raphael Bocco aliyeumia katika Robo
Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya El Merreikh ya
Sudan mwezi uliopita, naye anatarajiwa kuanza mazoezi mapema wiki
ijayo.
Tayari majeruhi mwingine wa muda mrefu wa Azam FC, Waziri Salum ameanza mazoezi tangu mwishoni mwa wiki.
Home
MICHEZO
DOMAYO WA AZAM ATAANZA KUJIFUA OCTOBA 1 BAADA YA KUMALIZA MUDA WA MAPUMZIKO KUFUATIA KUFANYIWA UPASUAJI WA NYAMA ZA PAJA ##
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment