BOSI
wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa Timu yake ilikuwa mdebwedo huko
Signal Iduna Park Jumanne Usiku ilipopigwa Bao 2-0 na Borussia Dortmund
katika Mechi ya kwanza ya Kundi D la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Bao toka kwa Ciro Immobile na Pierre-Emerick Aubameyang zimewaacha Arsenal wakiwa mkiani mwa Kundi D baada ya Mechi nyingine ya Kundi hilo, kati ya Anderlecht na Galatasaray kumalizika kwa Sare.
Baada kuzidiwa kila kitu huko Germany na kunusurika kupigwa lundo la Magoli, Arsene Wenger amekiri Timu yake ilikosa bahati Kipindi cha Kwanza lakini kwa ujumla ilizidiwa kila kitu.
Wenger amesema: “Nadhani hatukuwa kwenye kiwango chetu Usiku huu. Walistahili kushinda.”
Hata hivyo, Wenger amedai walikosa bahati kwani Bao la Kwanza walifungwa Sekunde 10 tu kabla ya Haftaimu.
Vile vile, Wenger alimtetea Straika wake mpya waliemnunua kutoka Manchester United, Danny Welbeck, ambae licha ya kuhangaika sana na kucheza vizuri, alikosa Bao za wazi kadhaa.
Wenger alieleza: “Welbeck alikuwa hatari lakini alichoka Kipindi cha Pili. Ndio maana hakumaliza lakini alicheza vizuri. Anahitaji Goli ili atulie.”
Mechi inayofuata kwa Arsenal kwenye Kundi D la UCL ni hapo Oktoba Mosi dhidi ya Galatasaray Uwanjani Emirates.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RATIBA – KUNDI D
Jumatano Oktoba 1
**Mechi kuanza Saa 2145 Bongo Taimu
Arsenal v Galatasaray
Anderlecht v Borrussia Dortmund

0 comments:
Post a Comment