PAUL SCHOLES ametoboa jinsi Sir Alex Ferguson alivyokuwa akipanga
mikakati ya kila Mechi za Manchester United wanazokabiliana nazo na
kusema hata Mechi ndogo yeye alizichukulia kama ‘Fainali ya Kombe la
Dunia.’
Scholes, ambae sasa amestaafu kucheza Soka baada ya kuitumikia Man
United katika maisha yake yote ya Soka na kucheza Mechi 499 chini ya Sir
Alex Ferguson, amesema Ferguson alijua mno namna ya kuongea na
kuhamasisha.
Scholes amesema: “Siku za Mechi Uwanjani Old Trafford tulifika Saa 6
na nusu Mchana na Sir Alex alionana na kila Mchezaji mmoja mmoja Ofisini
kwake. Mara nyingine alikwambia huchezi Mechi hiyo na mara nyingine
alikuelekeza nini anataka ufanye katika Mechi hiyo.”
Baada ya hapo Kikosi kizima kilijumuika kwa Mkutano wa pamoja ambao
pia ulipitia kuchambua Video za Wapinzani wao wa Siku hiyo kwa Muda wa
Dakika 10.
Scholes ameeleza: “Sir Alex alikuwa na uwezo wa kuzifanya Mechi
ndogo, kama zile za Raundi ya mwanzo za FA CUP na zile dhidi ya Timu za
chini za Ligi zionekane kama ni Fainali ya Kombe la Dunia!”
Aliongeza: “Mazungumzo yake yanakuingia kichwani na kukuhamasisha!”
Hata hivyo, Scholes alibainisha si mara zote Ferguson alikuwa
akifanya matayarisho kwa aina hiyo kwani kuna wakati alikuja na kutamka
Sentensi moja tu.
Scholes amesema: “Mara chache, si Mechi kubwa, tulikuwa tukimngoja na
anaingia akionekana na hasira. Halafu hutoa amri: ‘Nendeni mkaifunge
Timu hii! Sentensi moja tu na huyo katoka!”

0 comments:
Post a Comment