SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LIMESHAURIWA KUBORESHA MFUMO WAKE WA TIKETI ZA ELEKTRONIC ##


Shirikisho la soka nchini (TFF) limeshauriwa kuboresha mfumo wake wa tiketi za elektronic  usiwe na usiri wa mapato
yanayopatikana wakati wa mechi na pia malipo kwa wato huduma yatolewe haraka.

Ushauri huo ulitolewa jana na Meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga,Mbwana Msumari alipokuwa akizungumzia  kuhusiana na mapato ya mchezo uliofanyika jumamosi iliyopita baina ya Mgambo Shooting na Kagera Suger.
kulia ni Meneja wa uwanja huo,Mbwana Msumari.
Alisema hadi jana Alhamisi,uongozi wa uwanja huo haukuwa ukifahamu ni kiasi gani cha mapato yaliyopatikana kutokana na mchezo huo kwa sababu ya utaratibu uliowekwa na mfumo huo kuwa wa siri.

Meneja huyo pia alisema hata watoa huduma katika mchezo huo hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo limesababisha uongozi wa uwanja huo kuingia katika mgogoro wa kudaiwa.

"Siyo kwamba tunapinga mfumo wa tiketi za elektroniki,la hasha  tunautaka kwa sababu umeondoa mianya ya upotevu wa mapato ilia tunashauri uboreshwe"alisema Msumari.

Meneja huyo alieleza kushangazwa kwake na kitendo cha maafisa wa mfumo huo kutupa mapendekezo yaliyotolewa na wadau wakati walipowasili Tanga kuwaendeshea semina.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment