TIBAIJUKA AOMBWA KUINGILIA KATI MGOGORO ENEO LA VIWANDA KANGE TANGA ##

Wamiliki wa  eneo la viwanda la Kange Jijini Tanga wamemuomba Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi,Profesa Anna Tibaijuka kuingilia kati mgogoro wa uvamizi eneo lao  kabla ili kuepusha uwezekano wa kutokea uvunjifu wa amani.

Wamesema eneo lao ambalo walimilikishwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga tangu 2008 ,limevamiwa na Serikali ya Kijiji cha Kichangani na kugawa  kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kinyume cha sheria.

Katibu wa kamati ya  walimiki hao wa viwanda ya kushughulikia mgogoro huo,Kassim Salim alisema jana kuwa umefikia hatua mbaya  na sasa kuna hatari ya kumwagika damu  kwa sababu vijana wa Kichangani wanazuia mwamiliki wa viwanda kujenga hapo.

“Baadhi tunataka kujenga viwanda lakini kuna vijana wamekuwa wakizuia magari kumwaga mawe na mchanga,ina maana wamejipanga kwa vurugu  sasa hii hali inatakiwa kuingiliwa kati”alisema Salim.

Katibu huyo alisema tayari wamiliki hao wamefikisha malalamiko yao katika ngazi mbalimbali za Halmashauri ya Jiji na Serikali Wilaya ya Tanga lakini kuna hali ya kutegeana kutoa maamuzi jambo ambalo linaweza kuhatarisha hali ya amani katika eneo hilo.

Alisema ili kuleta hali ya amani katika en eo hilo wameona ni vyema
kumuomba Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Anna Tibaijuka kuingilia kati.
  
Mwenyeikiti wa Serikali ya Kijiji cha Kichangani,Rajab Mbalazi alisema kimsingi katika eneo hilo hakuna mgogoro kwa sababu ni mali ya Kijiji na imeamua kugawa kwa wananchi kwa kufuata taratibu zake na kwamba,wamiliki hao waligawiwa kinyume cha sheria kwani si mali ya Halmashauri ya Jiji.

“Mwaka 2008 Halmshauri ya Jiji la Tanga kupitia idara yake ya mipango ilichukua ardhi hiyo kinyemela bila ridhaa ya kijiji ndipo mwaka 2012 kupitia mkutano mkuu wa kijiji ukaamua kurejesha ardhi yake”alisema
Mbalazi.

Mwenyekiti huyo alisema kuanzia Julai 28 mwaka 2012 Serikali ya kijiji iliamua kutekeleza kwa vitendo na karibu asilimia 90 ya ardhi iliyokuwa imechukuliwa na halmashauri ya jiji kinyemela tayari
imeshagawa kwa wananchi.

Hata hivyo ipo  nakala ya tangazo lililotolewa na Halmashauri ya Jiji la Tanga lililosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji,Juliana Malange likitahadharisha kwamba kumejitokeza watu au kikundi chenye tabia  ya uvamizi katika viwanja  katika maeneo ya Kange  A,B,C,D,E,F  na Kange eneo la Viwanda ,Masiwani shamba,Mwakidila,Mwahako,Magaoni,Mwambani,Mbugani na EPZ.

Tangazo hilo liliwatahadharisha wananchi kuepuka kununua  ovyo viwanja ambavyo havina  nyaraka  halali huku likiwahimiza wenye viwanja kuvilinda.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment