JUMANNE SEPTEMBER 30
KUNDI E
PFC CSKA Moskva v FC Bayern München
-Mwaka Jana, CSKA walitolewa na Bayern kwa kuchapwa 3-1 kwao Moscow baada kupigwa 3-0 huko Munich.
Manchester City FC v AS Roma
-Mara ya mwisho kwa Man City kuifunga Klabu ya Italy ni Msimu wa
1978/79 walipoichapa 3-0 AC Milan kwenye Raundi ya Tatu ya UEFA Cup na
kuibwaga nje kwa Jumla ya Bao 5-2 kwa Mechi mbili.
KUNDI F
APOEL FC v AFC Ajax
-Ajax hawajashinda Ugenini katika Mechi 7 za UEFA CHAMPIONZ LIGI na
mara ya mwisho kushinda ni Oktoba 2011 walipoichapa GNK Dinamo Zagreb
Bao 2-0.
Paris Saint-Germain v FC Barcelona
-Klabu hizi zina uhusiano kwa baadhi ya Watu wake wa sasa kwani
Makocha Laurent Blanc wa PSG na Luis Enrique wa Barcelona walicheza
pamoja huko Nou Camp kwenye Msimu wa 1996/97.
Nae Staa wa PSG, Zlatan Ibrahimović, alikuwa huko Barca Msimu wa
2009/10 na kutwaa Vikombe Vinne na kufunga Bao 16 katika Mechi 29 za La
Liga.
Nao Thiago Motta na Maxwell, wote wa PSG, wameshawahi kuichezea Barca.
KUNDI G
Sporting Clube de Portugal v Chelsea FC
-Sporting wameshinda Mechi zao 3 zilizopita za Nyumbani dhidi ya
Klabu za England bila kufungwa hata Bao na kipigo chao pekee ni Msimu wa
2007/08 kwenye Mechi ya Kundi la UCL walipofungwa 1-0 na Manchester
United.
FC Schalke 04 v NK Maribor
-Maribor hawajawahi kuifunga Klabu yeyote kutoka Germany katika Mechi 4 za Mashindano ya Ulaya.
KUNDI H
FC Shakhtar Donetsk v FC Porto
-Porto, kwenye Mechi ya Kundi ya Msimu wa 2011/12 waliifunga Shakhtar
huko Ukraine Bao 2-1 kufuatia ushindi wao wa Nyumbani wa 2-1.
FC BATE Borisov v Athletic Club
-BATE, ambao wamefungwa Mechi zao zote 8 dhidi ya Klabu za Spain
kwenye Mashindano ya Ulaya, watacheza Mechi hii kwa mara ya kwanza Mjini
kwao Donetsk baada ya Mechi zao 9 zilizopita ambazo walikuwa wakiutumia
Mji wa Minsk.
Jumatano Oktoba 1
KUNDI A
Club Atlético de Madrid v Juventus
-Atlético walishinda Mechi 5 kati ya 6 walizocheza Nyumbani za UCL
Msimu uliopita na wameshinda Mechi 17 kati ya 19 zilizopita walizocheza
Uwanjani kwao Vicente Calderón kwenye Mashindano ya UEFA.
Malmö FF v Olympiacos FC
-Hii ni Mechi ya kwanza kwa Malmö kucheza Nyumbani kwenye UCL na hii ni mara ya kwanza kukutana na Klabu kutoka Ugiriki.
KUNDI B
PFC Ludogorets Razgrad v Real Madrid CF
-Msimu uliopita, Real Madrid, kwenye UCL, walifunga Jumla ya Bao 20
katika Mechi 6 za Ugenini waliposhinda Mechi 4 na Kufungwa 1 tu na
Borussia Dortmund Bao 2-0 kwenye Robo Fainali.
Mechi mbili katika hizo walizoshinda, waliweka Rekodi ya Klabu yao ya
Bao nyingi walipozitwanga 6-1 Galatasaray AŞ katika Mechi ya Kundi na
FC Schalke 04 katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
FC Basel 1893 v Liverpool FC
-Msimu wa 2002/03 kwenye Mechi ya Makundi ya UCL, Basel ilitoka Sare
1-1 na Liverpool huko Anfield na katika Mechi ya Marudiano huko Uswisi
waliongoza Bao 3-0 lakini Liverpool wakasawazisha na Gemu kwisha 3-3.
KUNDI C
FC Zenit v AS Monaco FC
-Zenit wana Rekodi nzuri Nyumbani kwao Petrovsky Stadium kwa kushinda
Mechi 30 kati ya 48 na kupoteza 3 tu katika Kipindi cha Miaka 12.
Bayer 04 Leverkusen v SL Benfica
-Benfica walishinda Mechi zote mbili walipokutana na Bayer 04
Leverkusen Msimu wa 2012/13 wa Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA
LIGI kwa kushinda 1-0 huko Germany na 2-1 Nyumbani kwao.
KUNDI D
Arsenal FC v Galatasaray AŞ
-Mara pekee Timu hizi kukutana ni kwenye Fainali ya UEFA CUP Msimu wa
1999/2000 huko Copenhagen, Denmark na kutoka Sare 0-0 katika Dakika 120
za Mchezo na Galatasaray kutwaa Kombe kwa Penati 4-1.
RSC Anderlecht v Borussia Dortmund
-Timu hizi zilikutana kwenye Msimu wa 1990/91 katika Raundi ya Tatu
ya UEFA CUP na Anderlecht kufuzu kwa Bao la Ugenini baada kushinda 1-0
Nyumbani na kufungwa 2-1 Ugenini.
RATIBA MECHI ZITAKAZOFUATA
JUMANNE SEPTEMBER 30
KUNDI E
1900 CSKA Moscow VS Bayern Munich
21:45 Man City VS Roma
KUNDI F
21:45 APOEL Nicosia VS Ajax
21:45 Paris St-Germain VS Barcelona
KUNDI G
21:45 FC Schalke 04 VS NK Maribor
21:45 Sporting Lisbon VS Chelsea
KUNDI H
BATE Borisovs VS Athletic Bilbao
Shakhtar Donetsk VS FC Porto
KUNDI A
21:45 Atlético Madrid VS Juvsentus
21:45 Malmö FF VS Olympiakos
KUNDI B
21:45 FC Basel VS Livserpool
21:45 Ludogorets Razgrad VS Real Madrid
KUNDI C
1900 Zenit St Petersburg VS Monaco
21:45 Bayer 04 Levserkusen VS Benfica
KUNDI D
21:45 Arsenal VS Galatasaray
21:45 RSC Anderlecht VS Borussia Dortmund
0 comments:
Post a Comment