Hayo yamezungumzwa katika mahojiano maalum kuihusu kauli ya Jaji Warioba kuwa atapambana na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta mitaani kuhusu
mabadiliko yaliyofanywa kwenye Rasimu ya Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha
kuhifadhi Falsafa za Mwalimu Nyerere, Dr. Muzamil Kalokola amesema kauli za
Jaji Warioba zinaonyesha hali ya kutatapa na anajivunjia heshima kwa
kuendeleza malumbano hayo.“Hakupaswa kuzungumza hivyo na kwanza amekiuka kiapo alichukula cha Utii na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,” alisema Dr. Kalokola ambaye alimtaka Jaji Warioba kama anataka kujiingiza katika siasa atangaze upande anaopendelea.
Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa si vyema kwa mtu mwenye heshima kama Warioba kuanza kuonekana akitetea kwa nguvu Rasimu ambayo anadai ni ya wananchi badala yake anatakiwa aache mchakato uende kama ilivyopangwa.
Dr. Kalokola alisema kuwa anaamini kuwa matatizo yanayojitokeza sasa yametokana na Jaji Warioba kutokufuata utaratibu unaotakiwa katika kukusanya na kuandika rasimu ya Katiba.
“Kinachotokea hivi sasa kimetokana na yeye mwenyewe, anapoitetea rasimu kwa kupiga kelele moja kwa moja tunapata wasiwasi kama ilikuwa mawazo ya wananchi kiukweli. Kama angefuata taratibu na hadidu za rejea basi tatizo hili lisingekuwepo.
Dr. Kalokola ambaye alifungua kesi dhidi ya Tume juu ya mchakato wa Katiba alimtaka Jaji Warioba kuhudhuria mwenyewe katika kesi hiyo badala ya kumtumia Wakili wa serikali kama anataka kupambana moja kwa moja na kutetea rasimu yake.

0 comments:
Post a Comment