Klabu
ya Congo DR, AS Vita, Jana imeifunga Klabu ya Tunisia Bao 2-1 katika Mechi ya
Marudiano ya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa huko Tunis, Tunisia
na sasa wametinga Fainali kwa Jumla ya Bao 4-2 baada kushinda Mechi ya Kwanza
pia 2-1.

Klabu ya Congo DR, TP Mazembe, Leo Uwanjani kwao Stade TP Mazembe Lubumbashi
imeifunga Entente Sportive de Sétif ya Algeria Bao 3-2 katika Mechi ya
Marudiano ya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI lakini imetupwa nje kwa Bao za
Ugenini
Katika Mechi ya Kwanza, ES Setif iliifunga TP Mazembe Bao 2-1 na hivyo Jumla
ya Magoli kwa Mechi mbili kuwa 4-4 na Setif kutinga Fainali kwa ubora wa Bao za
Ugenini.
Kwenye Fainali, ES Setif watacheza na Klabu nyingine ya Congo DR, AS Vita,
ambao Jana waliifunga Club Sportif Sfaxien ya Tunisia Bao 2-1 na pia kushinda
Mechi ya kwanza kwa Bao hizo hizo.
Hadi Mapumziko TP Mazembe walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao za Daniel Nii
Adjei
na Coulibaly na Setif kufunga Bao lao kupitia Abdelmalek Ziaya.
Kipindi cha Pili, Bolingi aliipa TP Mazembe Bao la 3 na hadi hapo Klabu hiyo
ya Lubumbashi ilikuwa ipo Fainali lakini Dakika ya 75 Younes Sofiane aliwakata
maini kwa kuifungia Setif Bao la Pili.
Hadi mwisho TP Mazembe 3 ES Setif 2.
Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI itachezwa kwa Mechi mbili, Nyumbani na
Ugenini, hapo Wikiendi ya Oktoba 25 na Marudiano Novemba 1.
FAINALI
0 comments:
Post a Comment