YANGA SC imefanya kali yake leo baada ya ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara baada ya kuichapa Prisons
ya Mbeya mabao 2-1 .
Mbrazil Andrey Coutinho alikuwa wa kwanza kuipatia
Yanga SC bao dakika ya 34 Kwa ujumla, Yanga SC inayofundishwa na Mbrazil
Marcio Maximo, ilicheza vizuri kipindi cha kwanza, wakati Prisons pamoja na
kuonyesha upinzani, lakini ilioneiana kuzidiwa.
Prisons ilikwenda mapumziko ikiwa pungufu, baada ya beki wake, Jacob
Mwakalobo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 39 baada ya kuonyeshwa kadi ya
pili ya njano na refa Andrew Shamba wa Pwani, kufuatia kumchezea vibaya Ngassa.
Kipindi cha pili, Prisons wakasawazisha dakika ya 67, mfungaji Ibrahim
Kahaka aliyetokea benchi ambaye alimalizia pasi ya Jeremiah Juma.
Dakika mbili baadaye, Simon Msuva aliifungia Yanga
SC bao la ushindi akimalizia krosi maridadi ya Ngassa .
WACHEZAJI WA YANGA : ; Deo Munishi ‘Dida’, Juma
Abdul, Edrwad Charles, Kevin Yondan/Rajab Zahir dk77, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga/Hamisi Thabit dk54, Genilson
Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Simon Msuva dk58.
WACHEZAJI WA
PRISONS: Mohamed Omar, Salum Lameya, Laurian Mpalile/Boniface Hau dk74, Nurdin
Chona, Lugano Mwangama, Jumanne Elfadhil, Meshack Olest/Julius kwangwa dk35,
Freddy Dungu, Jacob Mwakalobo, Amin Omary/Ibrahim Kahaka dk53 na Jeremiah Juma.
0 comments:
Post a Comment