
Hivyo timu hiyo italazimika kuingia
uwanjani hapo kama Simba aliyejeruhiwa ili kuhakikisha inapata matokeo mazuri
kwao ndani ya dakika 90 za mchezo huo.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa
Benchi la Ufundi la timu hiyo,Muhibu Kanu ambapo alisema kuwa timu hiyo ina
deni ambalo linapaswa kufanyiwa kazi ipasavyo kwenye mechi yao hiyo ya leo ili
waweze kutimiza matakwa yao.
Akizungumzia maandalizi ya timu
hiyo,Kanu amesema kuwa kikosi chao kipo imara kwa ajili ya kufanya vizuri ili
kuweza kusongea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo kutokana na
mapungufu walioyafanyia kazi kwenye mechi yao iliyopita dhidi ya Nanda FC na
kukubali kichapo cha bao 4-1.
Amesema kuwa kwenye mchezo huo
wachezaji wao watano waliokosa mchezo huo ambao walikuwa majeruhi tayari
walikwisha kupona na wapo imara kuweza kucheza kwenye mechi hiyo ya leo.
Amewataja wachezaji hao ambao
hawakuonekana kwenye mchezo wao uliopita na wapo tayari kupambana kuhakikisha
ushindi unapatikana kuwa ni Mohamed Soudy,Iddy Moby,Roberty Magadula,Mohamed
Jingo na Hamadi Juma (ambaye alikuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya vijana
ya Tanzania).
“Kama ujuavyo sisi
tunapaswa kupambana vilivyo ili kuweza kupata matokeo mazuri kwa sababu mechi
yetu ya kwanza tulipoteza mchezo huo hivyo ni lazima kushinda kwani tunakumbuka
sana kauli ya tuliomuhaidi pia Mbunge wetu Steven Masele kushinda mechi za
nyumbani na ugenini “Amesema Kanu.
Stand United ilishafika mkoani
lakini ikaamua kujichimbia wilayani Korogwe Kabla ya kutua jijini Tanga jana
jioni kwa ajili ya mazoezi kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani.
Wakati huo huo,Kocha Mkuu wa timu ya
Mgambo Shooting,Bakari Shime amesema kuwa wimbi uliotumika kuwakata Kagera
Sugar kwenye mechi ya Ufunguzi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ndio
atakaoutumia kwenye mechi hiyo.
Shime ameyasema hayo mara baada ya
kumalizika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye viwanja vya Kange Jeshini
jijini hapa ambapo alisema wao wamejipanga vilivyo wanashinda mechi zote
zilizopo mbele yao.
Akizungumza hali ya wachezaji,Kocha
Shime amesema kuwa kikosi chake kipo vizuri na hakuna majeruhi wa aina yoyote
na kuwahaidi ushindi wapenzi na mashabiki wake.
0 comments:
Post a Comment