Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group Limited imejitokeza kuwa mdhamini
mshiriki wa tuzo hizo kwa kutoa Sh. Milioni 10.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam katika hafla ya kutangaza udhamini
huo jana, Meneja Mkuu wa SSB Limited, Said Muhammad Said alisema wameamua
kudhamini tuzo hizo kama hatua mojawapo ya kuinua michezo nchini.
Aliupongeza uongozi wa TASWA kwa juhudi kubwa
inazofanya katika kuhamasisha michezo na kwamba wameona waunge mkono juhudi
hizo kwa kutoa fedha hizo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA, Juma
Pinto alisema kampuni mbalimbali zimeonesha nia ya kudhamini tuzo hizo na
watakuwa wanazitangaza kadri watakavyomalizana nazo.
![]() |
Juma Pinto |
“Bajeti ya tuzo zetu ni Sh milioni 120, zipo
kampuni zimeonesha nia ya kutusaidia, mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa
wiki ijayo tutatangaza wadhamini wengine,” alisema Pinto.
UNAWEZA KUSIKILIZA HAPA..
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TASWA, Amir
Mhando alisema Kamati Maalum ya Tuzo hizo inaendelea na mchakato wake wa kupata
wanamichezo hao na kwamba kadri watakavyokuwa wanapiga hatua watatoa taarifa
kwa wanahabari.
Alisema maandalizi mengine yanaenda vizuri na
wanaamini zitakuwa tuzo bora kuliko zote zilizowahi kufanywa na chama hicho
katika miaka ya hivi karibuni.
Kwa miaka mitano iliyopita walioshinda Tuzo ya
Mwanamichezo Bora wa TASWA walikuwa ni
Samson Ramadhani (2006), Martin
Sulle (2007), Mary Naali (2008), ambao wote ni wanariadha,
wakati 2009 na 2010 alikuwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan na mwaka 2011
alikuwa beki Shomari Kapombe ambaye sherehe za kumkabidhi tuzo zilifanyika Juni
mwaka 2012. Mwaka jana tuzo hizo hazikufanyika.
Wakati huohuo, Mhando alisema chama chake
kinaendelea na mazungumzo na wadhamini mbalimbali kuhusiana na tamasha kwa
ajili ya vyombo vya habari ‘Media Day Bonanza’ na kwamba mapema mwezi ujao
suala hilo litakuwa limemalizika.
0 comments:
Post a Comment