BONDIA ALLEN KAMOTE WA TANGA JANA AMEFANIKIWA KUIBUKA NA UBINGWA WA DUNIA WA (UBO) BAADA YA KUMSHINDA KWA POINTI MPINZANI WAKE OSGOOD KAYUNI WA MALAWI ##

BONDIA Allen Kamote wa Tanga jana amefanikiwa kuibuka na Ubingwa wa Dunia wa (UBO) baada ya kumshinda kwa pointi mpinzani wake Osgood Kayuni wa Malawi katika pambano la raundi kumi na mbili lenye uzito wa kg  61 ambalo lilifanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga  sikukuu
ya Eid El Haj.
 
Katika mapambano mengine yaliyochezwa ya utangulizi  Bondia Jacob Maganga na Said Mundi walishindwa kutambiana wakiwa ulingoni baada ya kumaliza mpambano wao huo wa na umwamba wa kutupiana makonde mpaka mwisho wa mpambano matokeo ni droo.
Awali katika mapambano ya utangulizi Bondia Fransic Miyeyusho alishinda kwa pointi zidi ya Emilio Norfat kutoka mkoani Arusha ambapo pambano hilo lilikuwa na biurudani ya aina yake kutokana na mabondia hao kucheza ngumi kwa umakini mkubwa.

Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment