Mjumbe wa
bunge maalumu la Katiba kutoka wajumbe wa 210 Juma Khamis Faki ametaka wananchi
wa Zanzibar waipitishe Rasimu ya Katiba
iliyopitishwa na Bunge huku akifafanua kwamba imelenga katika kuzipatia
ufumbuzi kero zinazoukabili Muungano .
Amesema kuwa Rasmu iliyopitishwa na Bunge maalumu la katiba ni mkombozi kwa wananchi wa Bara la Visiwani na kuongeza kwamba atashangaa kuwaona wanaikwamisha rasmu hiyo ambayo inaonekana kuwanufaisha wananchi wa Tanzania .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika uwanja wa Ndege wa Karume Chake Chake baada ya kuwasili Kisiwani Pemba ikitokea Dodoma , mjumbe huyo kutoka Chama cha UDP amewataka wananchi kutohadaiwa na baadhi ya wanasiasa wasiojali maslahi ya umma .

Amesema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa wanaibeza rasimu hiyo na kubainisha kwamba hao ni wanasiasa wasiojali maslahi ya umma na badala wanajali zaidi maslahi yao binafsi .
Aidha Mjumbe huyo amesema kuwa kazi kubwa ya wanasiasa iliyobaki ni kuwaelimisha wananchi juu ya rasimu hiyo na kuahidi kwamba ataitumia fursa yake kuhakikisha kwamba anawaelimisha wananchi na wanakuwa na elimu ya kutosha juu ya rasimu hiyo .
Akizungumzia tuhuma ambazo amekuwa akituhimiwa na baadhi ya wanasiasa kwamba juu ya msimamo wake , kwenye Bunge hilo amesema kuwa yeye ameenda katika bunge kwenda kutetea maslahi ya wananchi wa Zanzibar .
0 comments:
Post a Comment