TIMU
ya Coastal Union imeendelea kujimarisha katika maandalizi ya kuelekea mechi yao
na Mgambo Shooting inayotarajiwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani
ikiwa ni muendelezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Coastal Union imekuwa ikifanya mazoezi mara moja kila siku kwenye viwanja vya
Shule ya Sekondari Popatlaly ikijiwinda na mechi zake za Ligi hiyo ambayo msimu
huu inaonekana itakuwa na upinzani mkubwa.
Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa kikosi chake kimeimarika vilivyo ili kuweza kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu kila mchezo lengo likiwa kumaliza ligi mzunguko wa kwanza wakiwa kwenye nafasi za juu.
0 comments:
Post a Comment