MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) IMEZINDUA RASMI ZOEZI LA UTAMBUZI NA USAJILI WA WATU KATIKA MKOA WA TANGA ##

Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Watendaji katika ngazi zote Tarafa, Kata, Mitaa, Vijiji na Vitongoji, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Vyama vya Siasa wameagizwa kuonyesha ushirikiano  katika kuhakikisha jukumu la utambuzi na usajili wa watu linaenda sawasawa na maagizo ya Serikali .

Msisitizo huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa ambaye ameahidi kutoa ushirikiano wakati akizindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili wa watu uliofanyika mapema leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akizindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili wa watu.

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Salum Mohamed Chima ( Alhaji) akizunguza muda mchache kabla ya uzinduzi.

Bw. Joseph Makani, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) akizungumza wakati wa uzinduzi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa ,  Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw.Salum Mohamed Chima (Alhaj) na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Halima Dendego
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho( NIDA) Bw. Joseph Makani amewataka wakazi wa Tanga kujitokeza na kutoa ushirikiano katika zoezi zima kwani zoezi  hilo Mkoani Tanga ni utekelezaji wa Mpango wa Usajili wa Wakazi waishio Kihalali Nchini kwa lengo la kuwapatia vitambulisho vya Taifa kwa hadhi ya raia, Wageni wakazi na Wakimbizi.

Baadhi ya viongozi wawakilishi kutoka katika Wilaya za Tanga wakati wa uzinduzi

“Fichueni wale ambao hawastahili kupata vitambulisho vya uraia kwa kutoa taarifa katika ofisi za uhamiaji na polisi ili taifa lisije likaingia katika hatari ya kuwasajili wageni kama raia”amesisitiza Makani.

 Zoezi la Utambuzi na Usajili Mkoani Tanga nilitegemea kuanza Oktoba 12 mwaka huu. Wananchi wanaombwa kuhakikisha wanajisajili kwa wenyeviti wa mitaa ili kurahisisha zoezi hilo. Stori & Picha na Monica Laurent, Afisa Habari Tanga.

KWA MAELEZO ZAIDI UNAWEZA KUSIKILIZA HAPA
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment