WAZIRI wa Nchi Ofisi
ya Rais Utawala Bora,George Mkuchika amewaagiza maafisa Takukuru kwenye
Halmashauri nchini kuhakikisha wanakwenda kukagua taarifa ya fedha
za miradi ya maendeleo jinsi zilivyotumika kwenye maeneo yaliyokusudiwa
ili kuweza kubaini hali halisi.
Hayo aliyasema wakati akizungumza kwenye kikao cha Ushauri wa Mkoa wa Tanga (RCC) ambapo alisema kuwa miradi mingi kwenye halmashauri hapa nchini imegauzwa kuwa sehemu za kuchukulia fedha kwa watumishi wasiokuwa waaminifu jambo ambalo linakwamisha shughuli za maendeleo.

Alisema kuwa jambo hilo linatokana na wasimamizi wakuu wa halmashauri wakiwemo wakurugenzi wa Halmashauri na wataalamu wanachangia kwa asilimia kubwa kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo inayoendeshwa kwenye maeneo yao hali inayopelekea kujengwa chini ya kiwango na kushindwa kudumu kwa muda mrefu.
“Kwenye suala hili hakuna jinsi lazima maafisa Takukuru kwenye halmashauri kuacha kukaa ofisini badala yake mhakikisha mnakwenda kuziangalia fedha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yenu kubaini mambo yanayokwenda nah ii itasaidia uwajibikaji kwa wahusika “Alisema Mkuchika.
0 comments:
Post a Comment