STENDI YA MABASI ILIYOFUNGULIWA NA JK YAGOMEWA TANGA, MADEREVA WAPAKI MAGARI YAO ENEO LA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU WA LAMORE ##

STENDI ya Mpya ya Mabasi iliyofunguliwa na Rais  Jakaya Kikwete iliyopoeneo la Kange jijini Tanga imegomewa kuhamiwa na madereva wanaofanya safari zao kati ya Lushoto, Muheza, Korogwe, Handeni kwa madai ya kutokuwa na huduma za msingi za kijamii ikiwemo Kituo cha Polisi.

Mgomo huo ulifanywa na mabasi aina ya Coaster yanayofanya safari zakekati ya Tanga mjini kwenda wilayani jana  yalilazimika kugoma kuhamiakwenye kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani kwa madai kutokupewa taarifa za kuhamia huko pamoja na kutokuwepo kwa mazingira mazuri kwa
wasafiri wakati wa utoaji huduma hizo.

Mgomo huo ulianza saa moja asubuhi mpaka saa tano asubuhi ambapo magari yanaayofanya safari zake kati ya Tanga,Korogwe,Lushoto,Muheza na Handeni walilazimika kuyapaki magari yao kwenye eneo la uwanja wa Lamore uliopo Masiwani jijini Tanga wakipinga kitendo cha kutakiwa kuhamia kwenye stendi hiyo mpya.

Kutokana na hali hiyo madereva hao walilazimika  kwenda eneo la Stendi ya mabasi mpya wakizuia magari mengine yaliyokuwa  wakitoka nje ya Tanga kutokiungia ndani ya stendi hiyo hali  iliyoleta usumbufu kwa
baadhi ya magari binafsi yaliyokuwa wakitumia  barabara iliyopo pembeni ya stendi hiyo kabla ya askari wakiwa na bunduki  kufika eneo hilo na kutuliza ghasia.


Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment