Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga
linawashikilia raia wawili wa kigeni kutoka nchini Nigeria kwa tuhuma za
kukutwa wakiwa na milipuko nane ya miamba ya madini pamoja na waya wa
kuunganisha milipuko hiyo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga,Fresser Kashai alithibitisha kutoka tukio hilo ambapo
alisema lilitokea Octoba 12 mwaka huu saa sana mchana huko Kijiji cha Kigwashi
Kata ya Mashewa Tarafa ya Magoma wilayani Korogwe .
Aliwataja
raia hao wa kigeni waliokamatwa kuwa ni Keneth Ekenee (31) na Ameki
Boniface(31) wakiwa nyumbani kwa mwenyeji wao Frank alimaarufu Miki ambaye
baada ya tukio hilo alikimbia akiwaacha wenyeji wake wakiwa hawajui pa kwenda.
Kwa
upande mwingine Mkulima mmoja na mkazi wa Morogoro Michael
Charles(28)amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na risasi 39 alizokuwa
akizisafirisha bila kuwa na kibali halali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tanga Frasser Kashai alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa
Oktoba 8 mwaka huu majira ya saa 5.00 asubuhi huko katika eneo la Maili kumi
Kata ya Segera wilayani Korogwe akiwa katika basi lenye namba za usajili T510
CLB aina ya Nissan Caravan akitokea Monduli mkoani Arusha kuelekea Morogoro.
Aidha
watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa
Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
0 comments:
Post a Comment