SIMBA SC imefungwa mabao 2-0 na Jomo Cosmos mjini Johannesburg
jioni hii .
Pamoja na kufungwa na timu hiyo ya Daraja la Kwanza, fahamu
kwamba Huo ni mchezo wa tatu kwa Simba SC katika kambi yake ya Afrika Kusini tangu
ilipofika huko Oktoba 8, mwaka huu kwa ajili
ya maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu
wao, Yanga SC Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wake wa kwanza, Simba SC ililazimishwa sare ya
bila kufungana na Orlando Pirates kabla ya kufungwa mabao 4-2 na Bidvest Wits.
Simba SC inatarajiwa kurejea Dar es Salaam Ijumaa tayari kwa
mchezo wa Jumamosi, unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
NANI MTANI JEMBE ? 2014 KITAELEWEKA KAMA KIPINDI KILICHOPITA?
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment