TAIFA STARS hii Leo huko Mjini Mbabane, Swaziland Uwanjani Somhlolo imetoka Sare ya Bao 1-1 na Timu ya Taifa ya Swaziland, Sihlangu, katika Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki.
Sihlangu walioongoza Kwa Bao 1-0 hadi Mapumziko na Stars kusawazisha kwa Bao la Thomas Ulimwengu Dakika ya 51.
Lakini Ulimwengu aliikosesha Stars ushindi baada yya kukosa Penati katika Dakika ya 72.
Huo ni mchezo wa 10 Nooij anaiongoza Stars tangu arithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen Apili mwaka huu, katika mechi tisa za awali, m alishinda tatu, sare tatu na kufungwa tatu.
Nooij alianza kwa sare ya 0-0 na Malawi katika mchezo wa kirafiki mjini Mbeya, kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Zimbabwe mchezo wa kufuzu AFCON mjini Dar es Salaam.
Akashinda tena 1-0 na Malawi katika mchezo wa kirafiki Dar es Salaam kabla ya sare ya 2-2 na Zimbabwe kufuzu AFCON mjini Harare na baadaye kufungwa 4-2 na Botswana katika mchezo wa kirafiki mjini Gaborone.
Akatoa sare ya 2-2 na Msumbiji mjini Dar es Salaam kufuzu kabla ya mkwenda kufungwa 2-1 katika mchezo wa marudiano mjini Maputo na kisha kufungwa 2-0 na Burundi mchezo wa kirafiki mjini Bujumbura.
Mechi iliyopita, Nooij aliiongoza Stars kushinda kwa kishindo, mabao 4-1 dhidi ya Benin, ukiwa pia mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Said Mourad, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mwinyi Kazimoto, Thomas Ulimwengu, Juma Luizio na Amri Kiemba.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment