HALMASHAURI ZA MKOA WA TANGA ZIMETAKIWA KUHAKIKISHA WANAKUWA NA WAGANI AMBAO WATAWEZA KUSAIDIA KUTOA ELIMU KWA WAFUGAJI ##

Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa aliyehamishiwa mkoani Dodoma wakati akifunga mafunzo ya wafugaji wajasiriamali kutoka mikoa ya Pwani,Morogoro na Tanga yaliyofanyika mkoani hapa.


Alisema kuwa kimsingi wafugaji hao wanapokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu ufugaji wa kisasa utawasaidia kuongeza uzalishaji wao wa kila siku jambo ambalo litapelekea kuharakisha maendeleo yao pamoja na jamii zinazowazunguka.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Mkoani Tanga,Juma Mpimbi akisisitiza jambo kwa wafugaji wajasiriamali
Alisema kuwa kipato cha mkoa wa Tanga kitaongezeka kutokana sekta zote za uzalishaji ikiwemo Kilimo na Ufugaji kwa sababu asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa huo wanafanya shughuli kubwa hizo kwa ajili ya kupata kipato chao kutokana na kuwa ardhi ya mkoa inaweza kupandwa mazao ya  aina yoyote na yakaweza kustawi.

Aidha alisema kwenye sekta ya Maziwa hakuna shida ya masoko hivyo wafugaji wanapaswa kuongeza uzalishaji  wa kutosha ili waweze kuinua kipato chao kwa kufuata njia nzuri za ufugaji wa kisasa.

Aliongeza kuwa ili waweze kufanya biashara zao kwa ufanisi ambao utawapa mafanikio ya haraka haraka hawana budi kuhakikisha wanatafuta elimu itakayowapa mwanga mzuri wa kufuga kisasa hali ambayo itachangia kukuza wigo mpana wa masoko.

Hata hivyo alisema kuwa upo umuhimu mkubwa wa ardhi iliyopo mkoani Tanga ipimwe yote ili kuweza kuepusha migogoro isiyokuwa na tija ambayo inaweza kujitokeza baina ya wafugaji na wakulima jambo ambalo linarudisha nyuma kasi ya maendeleo ya wananchi.



Awali akisoma Risala kwa niaba ya washiriki wa mafunzo ya wafugaji wajasiriamali kutoka mikoa ya Pwani,Morogoro na Tanga,Rehema Salim alisema katika mafunzo hayo waliona kuwa ipo haja ya maafisa ugani kushirikiana na wafugaji kuwaelekeza namna ya kufuga kibiashara kwa kuomba watengewe bajeti ili watufikie na kutusimamia.

Rehema aliendelea kumuomba mkuu huyo wa mkoa kuhamasisha vyama vya msingi,vyama  vikuu vya  ushirika ngazi ya mkoa-TDCU ili viweze kuchangia gharama za mafunzo yao ikiwemo kuwawezesha kupata mafunzo kwa wakati pamoja na kutengewa bajeti ya mafunzo ya ujasiriamali.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment