WATU 14 WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA WENGINE 22 KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA ASUBUHI YA LEO WILAYANI MUHEZA MKOANI TANGA ##

WATU 14 wamefariki dunia papo hapo na wengine 22 kujeruhiwa  baada ya lori kuligonga gari la abiria aina ya Coaster eneo Mkanyageni wilayani Muheza mkoani Tanga ambapo Coaster hiyo inafanya safari zake kati ya Tanga na Lushoto.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Juma Ndaki alithibitisha kutokea tukio hilo ambapo alisema kuwa ajali hiyo  ilitokea majira ya saa moja na nusu asubuhi eneo la mkanyageni karibu na sehemu iliyokuwa na kona kali.

Akizungumzia jinsi ya ajali hiyo ilivyotokea, Ndaki alisema kuwa Dereva aliyekuwa akiendesha gari aina ya Coaster lililokuwa likitokea Tanga kwenda Lushoto alikuwa akilipita gari jengine lililokuwa mbele yake aliposhindwa na kutaka kurudi upande alipotoka alikutana na lori hilo ambapo katika harakati za kulikwepa akajigonga ubavuni.
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali wilayani Muheza wakitazama ajali ya Lori iliyohusisha gari aina ya Coaster na
kusababisha vifo vya abiria 14 na majeruhi 27
  
Kamanda Ndaki alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari aina ya Coaster ambaye alikuwa akilipita gari lilitokuwa mbele yake aina ya Coaster na aliposhindwa wakati akitaka kurudi upande wake ndipo alipokutana na lori hiyo na kusababisha ajali hiyo.
 


Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenda kutoa pole na wengine kuitambua miili ya ndugu zao



TRUSTED MISHEN  ilifika katika  hospitali hiyo na kujionea hali za majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu na wauguzi huku wananchi kutokana maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakijitokeza kuwatambua ndugu na jamaa zao kwa ajili ya taratibu nyengine.

Akizungumza   hospitalini hapo,Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Teule,Rajabu Malamhiyo alisema kuwa walipokea majeruhi 27 ,na waliokufa walikuwa 11 ambapo kati yao saba ni wanawake na wanne ni
wanaume ambao wamehifadhiwa kwenye chumba cha maiti kwenye hospitali hiyo.



Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment