NUNDU KUWA MGENI RASMI KATIKA ONESHO LA USIKU WA WAZEE NOVEMBA 30 TANGA ##

MBUNGE wa Jimbo la Tanga,Omari Nundu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onyesha maalumu ya usiku wa wazee ambalo linatarajiwa kufanyika Novemba 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Bandari.

Kamishna wa Scauti Mkoa wa Tanga,Modesta Kijazi amesema kuwa lengo la kuandaa onyesho hilo ni kuwaenzi wazee wa Jiji la Tanga na Mkoa mzima wa Tanga kwa kujaribu kukuza na kuendeleza mila na desturi.

Kijazi amesema katika onyesha hilo kutakuwa na mavazi ya asili ya zamani ambayo yatakuwa yakionyeshwa kwao pamoja na wadau wote watakaohudhuria siku hiyo ambayo imeandaliwa na chama cha Scauti wa Kike mkoa wa Tanga(Girl Guide).

Amesema kuwa licha ya kufanyika maonyesha hayo lakini pia kutakuwa na burudani za ngoma za asili ambazo zitakuwa ni taarabu asilia,muziki wa dansi na mziki mwengine wa zamani ambao utapewa nafasi ya kutumbuizwa siku hiyo.

Hata hivyo,Kamishna huyo aliwataka wazee wote waliopo mkoani Tanga kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuenziwa kwa kukumbushwa enzi zao za zamani.

Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment