UPO UWEZEKANO MKUBWA WA TIMU KUSAMBARATIKA MTU ASIPOFUZU LEO NGOMA NGUMU DIMBANI CITY NA BAYERN ##

MECHI ZA LEO JUMANNE
 
20:00 FC BATE Borisov - Belarus vs FC Porto - Portugal      
20:00 CSKA Moskva – Russia vs AS Roma - Italy       
22:45 Manchester City - England vs Bayern Munich - Germany       
22:45 Schalke 04 – Germany vs Chelsea FC - England
22:45 Paris Saint-Germain – France vs Ajax Amsterdam - Netherlands      
22:45 Apoel Nicosia – Cyprus vs FC Barcelona - Spain
22:45 FC Shakhtar Donetsk – Ukraine vs Athletic de Bilbao - Spain
22:45 Sporting Lisbon – Portugal vs NK Maribor - Slovenia  
++++++++++++++++++++++++++++
TIMU ZIZOFUZU KUINGIA RAUNDI YA MTOANO:
-Real Madrid CF
-FC Barcelona
-Paris Saint-Germain
-Borussia Dortmund
-FC Bayern München
-FC Porto
**BADO TIMU 10
**Timu zinazomaliza Nafasi ya 3 zinapelekwa EUROPA LIGI

++++++++++++++++++++++++++++

LEO USIKU Uwanjani Etihad Jijini Manchester, Mabingwa wa England Manchester City wana kimbembe kikubwa watakapombana na Mabingwa wa Germany Bayern Munich kwenye Mechi ya Kundi E la UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo City ni lazima washinde ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu yanayotaka pia washinde Mechi yao ya mwisho.

Leo City wanaivaa Bayern ambayo tayari imefuzu kucheza Raundi ya Mtoano ikiwa na Mechi mbili mkononi.

Mbali ya kuwa Mechi hii ni ngumu pia City wataingia Uwanjani bila ya Mastaa wao majeruhi, David Silva na Edin Dzeko na pia watamkosa Aleksandar Kolarov.

Bayern nao wana Listi ndefu ya majeruhi akiwemo Nahodha wao Philipp Lahm ambae atakuwa nje kwa Miezi Mitatu na wengine ni Claudio Pizarro, David Alaba, Holger Badstuber, Tom Starke, Pepe Reina, Javi Martinez na Thiago Alcantara.
++++++++++++++++++++++++++++
KUNDI E
MSIMAMO
KLABU
P
W
D
L
F
A
+/-
Pts
FC Bayern München
4
4
0
0
11
1
10
12
AS Roma
4
1
1
2
7
11
-4
4
PFC CSKA  Moscow                          
4
1
1
2
5
-9
-4
4
Manchester City FC
4
0
2
2
4
6
-2
2
++++++++++++++++++++++++++++
Ikiwa Man City watashindwa kushinda hii Leo na kwenye Mechi nyingine ya Kundi E kati ya CSKA Moscow na AS Roma akapatikana Mshindi basi City Leo hii watatupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Hii itakuwa ni mara ya 3 ndani ya Miaka Minne kwa City kushindwa kufuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kutoka hatua ya Makundi.

Hilo litakuwa balaa kubwa kwa Meneja Manuel Pellegrini na Wachezaji wake kwani Wamiliki wa City wametumia Pauni 750 Milioni kununua Wachezaji tangu walipotua City Mwaka 2008 na hamna mafanikio Ulaya.

Akiongelea kuhusu hili, Kiungo wa City, Samir Nasri, alisema: “Inabidi tufanye kitu au Mwakani watakuja Wachezaji wapya na kila kitu kipya. Tuwe wa kweli, kwa Mishahara ya Wachezaji na uwezo wa Asilimia 90 ya Wachezaji kutofuzu toka hatua ya kwanza ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ni pigo kubwa kwa Klabu na kwetu!”

MECHI ZA KESHO JUMATANO 
20:00 Zenit St. Petersburg – Russia vs Benfica - Portugal     
22:45 Arsenal FC – England vs BV Borussia Dortmund - Germany   
22:45 Atletico de Madrid – Spain vs Olympiacos CFP - Greece        
22:45 Bayer 04 Leverkusen – Germany vs AS Monaco FC - France  
22:45 FC Basel 1893 – Switzerland vs Real Madrid CF - Spain        
22:45 Malmö FF - Sweden vs Juventus FC - Italy       
22:45 RSC Anderlecht – Belgium vs Galatasaray Spor Kulübü - Turkey      
22:45 Ludogorets Razgrad – Bulgaria vs Liverpool - England
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment